Posts

Showing posts from March, 2020

Congo DRC yathibitisha kisa cha kwanza cha virusi vya Corona

Image
Kisa cha kwanza cha virusi vya Corona kimethibitishwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Msemaji wa wizara ya Afya amesema Jumanne. Mgonjwa huyo ni raia wa Ubelgiji ambaye alikuwa amewekwa karantini baada uchunguzi aliofanyiwa katika uwanja wa ndege wa Kinshasa kubaini kuwa ameambukizwa virusi hivyo.

Shonza atoa vifaa vya shilingi milioni 10 Songwe

Image
Naibu Waziri Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Juliana Daniel Shonza mapema leo ametoa vifaa mbalimbali vya michezo, Elimu na watu wenye Ulemavu vyenye thamani ya shilingi milioni 10,325,000 kwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe. Naibu Waziri Shonza ametoa Kompyuta Mbili, baiskeli mbili za watu wenye ulemavu, mipira na jezi kwa Brig. Jen. Nicodemus Mwangela huku akimpongeza kwa namna ambavyo amekuwa akiongoza jitihada mbalimbali za maendeleo ya Mkoa wa Songwe. “Nimeona nami nije kuunga Mkono jitihada za Mkoa kama Naibu Waziri lakini pia mbunge wa Mkoa wa Songwe, tunaziona Jitihada za Mkuu wa Mkoa katika kukuza sekta mbalimbali, napenda kuwaambia huu ni mwanzo tu name nitaendelea kuleta vitu mbalimbali.”, amesema Naibu Waziri Shonza. Aidha ameupongeza Uongozi wa Mkoa kwa kufanya maamuzi ya kununua timu ya Mpira wa Miguu itakayocheza ligi kuu ambayo itaweza kuuwakilisha Mkoa wa Songwe kitaifa na Kimataifa huku akiongeza kuwa Mkoa unafanya vizuri sana katika sekta ya Michez...

Iran yaathirika zaidi na Corona katika nchi za Mashariki ya kati

Image
Iran leo imesema watu 54 zaidi walioambukizwa virusi vya Corona wamefariki na kuifanya idadi jumla ya waliofariki kutokana na ugonjwa huo nchini humo kufikia 291. Kuna visa 8,042 vya maambukizi katika jamhuri hiyo ya kiislamu. Msemaji wa wizara ya afya Kianoush Jahanpour ametowa tangazo hilo kupitia mkutano na waandishi habari uliooneshwa kwenye televishhni. Idadi ya waliokufa iliyotangazwa leo inaonesha ongezeko la asilimia 18 ya vifo ikilinganishwa na siku moja iliyopita. Iran ndio nchi iliyoathirika kwa kiasi kikubwa na ugonjwa huo katika eneo la Mashariki ya kati. Katika eneo hilo kuna zaidi ya visa 8,600 vilivyothibitishwa vya maambukizi ya virusi hivyo. Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu nchini Iran Javaid Rehman ameitaka nchi hiyo kuwaachia huru kwa muda wafungwa wote wa kisiasa, akisema inasikitisha kuwa na wafungwa wa kisiasa katika kipindi hiki cha mripuko wa virusi vya Corona.

Rais Putin aunga mkono marekebisho ya katiba ya Urusi

Image
Rais Vladmir Putin wa Urusi amesema anaunga mkono pendekezo la marekebisho ya katiba ambayo yatamruhusu kugombea muhula mwingine wa kuendelea kukaa madarakani. Putin ameunga mkono mapendekezo hayo yaliyowasilishwa na mbunge ambaye wakati wa utawala wa Soviet alikuwa mwanamke wa kwanza kusafiri anga za mbali. Mbunge huyo amependekeza ama iondolewe kabisa sheria ya ukomo wa muhula wa rais madarakani au pafanyike marekebisho ya katiba yatakayomruhusu Putin agombee tena. Msururu wa marekebisho ya katiba ya Urusi yatapigiwa kura nchi nzima mnamo tarehe 22 mwezi Ujao wa Aprili. Rais Putin ameipinga hatua ya kuondolewa ukomo wa muhula wa rais lakini ameunga mkono fikra ya kufanyika marekebisho ya katiba.

Trump atarajiwa kutangaza mipango mipya ya kiuchumi

Image
Rais wa Marekani Donald Trump anajiandaa kutangaza mipango ya kiuchumi itakayotowa mwelekeo utakaochukuliwa na taifa hilo kufuatia kuenea kwa virusi vya Corona. Tangazo hilo linatolewa wakati masoko ya kiuchumi ya Marekani yakionesha kuporomoka kabla ya kufunguliwa kwa masoko. Miongoni mwa hatua zinazofikiriwa ni kuundwa kwa sheria ya kuwalinda wafanyakazi wanaolipwa kwa masaa ambao wako katika hatari ya kukosa mshahara kutokana na kuyumba kwa shughuli za kiuchumi au hatua za kufungiwa kwenye Karantini. Kadhalika rais Trump anafikiria hatua ya kuondowa kodi ya mshahara. Ama kwa upande mwingine waziri wa ulinzi wa nchi hiyo Mark Esper ameakhirisha ziara yake ya kwenda India,Uzbekistan na Pakistan ili kusaidia katika usimamizi wa wizara hiyo katika kupambana na virusi vya Corona.

VIDEO: Breaking News; Tazama msafara wa Mbowe na wenzake wakipelekwa gerezani

Image
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Freeman Mbowe wamelazimika kupelekwa gerezani baada ya kutokamilisha taratibu za faini ambazo wametakiwa kulipa. TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI......USISAHAU KUSUBSCRIBE

Mazishi ya Baba Kanumba Kufanyika Jumatano hii

Image
Siku ya Machi 8, 2020 zilitoka taarifa za kifo cha Baba wa aliyekuwa staa wa filamu hapa nchini Steven Kanumba, aitwaye Charles Kanumba, aliyefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Mkoa wa Shinyanga.  Happyness Charles ambaye ni mmoja wa watoto wa marehemu Baba Kanumba, akielezea kuhusu sababu ya kifo cha mzee huyo pamoja na ratiba kamili za mazishi ya msiba huo. "Taratibu za mazishi yenyewe yataanza  kesho Jumanne, ambapo tutaaga mwili wa marehemu kuanzia saa 8 mchana kisha kuelekea nyumbani kwao Busega Mwanza, ambapo tutazikia siku ya Jumatano mida ya saa 7 mchana, halafu tutarudi kumalizia msiba nyumbani kwake Shinyanga"  ameeleza Happyness Charles. "Baba ameanza kuumwa kichwa, tumbo na miguu kwa muda mrefu sana, alianza kuugua kabla ya Kanumba hajafariki kwa sababu alikuwa anaumwa polepole, kwahiyo kadri siku zinavyoenda hali inazidi kubadilika ghafla kisha akafariki" ameongeza

RC Tabora aagiza kukamatwa kwa wanaotumia vyandarua kinyume cha utaratibu

Image
MKUU wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amewaagiza viongozi wa vijiji na mitaa kuwamata watu wote watakutwa wakitumia vyandarua kwa matumizi mengine kando ya kujikinga na mbu. Alisema matumizi ya vyandarua nje ya kujikinga na mbu yanapingana na juhudi za Serikali za kupambana malaria na kusababisha kupoteza nguvu kazi ya Taifa Mwanri alitoa kauli hiyo  wilayani Kaliua wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Mkoa wa Tabora ziro malaria inaanza na mimi. Alisema kuwa katika baadhi ya watu wanatumia vyandarua kuvulia samaki katika madimbwi na wengine wanatumia kuzungushia vifaranga vya kuku vishismbuliwe na mwewe. Mwanri aliongeza kuwa kuna watu wengine wanatumia vyandarua hivyo kwa ajili ya kuzungushia bustani za matunda na mboga mboga ili kuzuia wadudu waharibifu. Alisema matumizi hayo ambayo ni kinyume cha kujikinga na mbu ni marufuku mkoani na atakayekuwa atachukuliwa hatua. Awali Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Honoratha Rutatatinisibwa alisema mwelekeo wa Serikali ni kuhakikisha...

Italia yachukua hatua za dharura nchi nzima kudhibiti virusi vya corona

Image
Italia imeongeza hatua za dharura za kupambana na maambukizi ya virusi vya corona, ikiwemo kuzuia safari na kupiga marufuku mikusanyiko ya Umma nchi nzima. Siku ya Jumatatu, Waziri Mkuu Giuseppe Conte aliamuru watu wabaki majumbani na sharti waombe ruhusa na kupata kibali kwa ajili ya safari zenye umuhimu pekee. Amesema hatua hizo ziliwekwa kwa ajili ya kuwalinda wale walio hatarini kupata maambukizi . ''Hakuna muda zaidi,'' alisema alipohutubia raia kwa njia ya Televisheni. Vifo vilivyotokana na virusi vya corona sasa vimefikia 463 kutoka 366 siku ya Jumatatu. Athari mbaya zaidi baada ya China. Idadi ya maambukizi imethibitishwa kufikia 24% kutoka siku ya Jumapili, maafisa walieleza. Visa vya maambukizi vimethibitishwa kuwepo kwenye miji yote 20 nchini Italia. Conte amesema hatua bora zaidi ni kuwa watu wasalie majumbani. ''Kuna ongezeko kubwa la maambukizi ...na vifo,'' amesema kwenye taarifa yake. Waziri Mkuu Conte ameeleza hatua hiyo inajulik...

Chama amuangukia Fei Toto

Image
Mchezaji wa Simba SC Clotous Chama amemuomba radhi mchezaji wa Yanga SC Feisal Salum kwa kumchezea rafu ya makusudi ambayo ingeweza kumtia jeraha kubwa katika mchezo wa derby jana. Chama amekiri kitendo hicho hakikuwa cha kiungwana Simba ikipoteza 1-0. “Nina huzuni tumepoteza lakini nataka niwahakikishie kwamba kilichotokea kati yangu na Feisal kilikuwa ni binafsi walasio kwa shinikizo la matokeo ya derby, binafsi nimeongea na Feisal na amekubali msamaha wangu”amesema Chama

Aston Villa yachapwa bao 4-0 na Leicester City

Image
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku wa jana amecheza kwa dakika zote 90, timu yake, Aston Villa ikiendelea kuvurunda katika Ligi Kuu ya England baada ya kuchapwa 4-0 na wenyej, Leicester City Uwanja wa King Power. Kipigo kinazidi kuiporomosha Aston Villa inayofundishwa na kocha Muingereza, Dean Smith sasa ikibaki na pointi zake 25 baada ya kucheza mechi 28 na kuendelea kukamata nafas ya 19, ikiizidi pointi nne Norwich City inayoshika mkia katika ligi ambayo mwisho wa msimu timu tatu zitateremka daraja. Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Michael Oliver, mabao ya Leicester City inayofundishwa na kocha wa zamani wa Liverpool, Brendan Rodgers yalifungwa na Harvey Barnes dakika ya 40 na 85 na Jamie Vardy mawili pia, dakika ya 63 kwa penalti na 79. Kwa ushindi huo, Leicester City inafikisha pointi 53 baada ya kucheza mechi 29 na kuendelea kukamata nafasi ya tatu, nyuma ya Manchester City yenye pointi 57 za mechi 28 na Liverpool yenye pointi 82 za mec...

Waziri mkuu wa Sudan arejea ofisini baada ya jaribio la kumuua

Image
Waziri Mkuu wa Sudan, Abdullah Hamdok amerejea ofisini leo mchana, saa chache baada ya jaribio la kumuua kushindwa kwenye mji mkuu wa nchi hiyo, Khartoum. Msemaji wa baraza la mawaziri, Faisal Mohamed Salih amesema kiongozi huyo anaendelea na majukumu yake ofisini kama kawaida. Hamdok ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba anawahakikishia watu wa Sudan kuwa yuko salama kabisa. Amesema shambulizi hilo halitorudisha nyuma harakati za Sudan kuelekea katika demokrasia. Faisal amesema vikosi vya usalama vinawatafuta magaidi walioushambulia msafara wa Hamdok. Shambulizi hilo lilitokea karibu ya gari la kiongozi huyo wakati msafara wale ukipita kuingia kwenye daraja la Kober, kaskazini mwa Khartoum akiwa anaelekea ofisini kwake. Hakuna kundi lolote ambalo limedai kuhusika na shambulizi hilo.

Hukumu ya Mbowe na viongozi wengine wa CHADEMA leo

Image
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo March 10, 2020 inatarajia kutoa hukumu kwa Viongozi wa CHADEMA, wanaokabiliwa na kesi ya uchochezi Mahakamani hapo. Viongozi wanaokabiliwa na shauri hilo ni pamoja na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, na Wabunge John Mnyika, Halima Mdee, Ester Bulaya, Ester Matiko, John Heche, Peter Msigwa na pia aliyekuwa Katibu Mkuu CHADEMA kabla ya kuhamia CCM, Vicent Mashinji. Hukumu hiyo inakuja baada ya February 24, 2020 Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba kusikiliza ushahidi wa upande wa mashtaka na ule wa utetezi na kutoa siku tano za kazi kwa Mawakili wa pande zote mbili kuwasilisha hoja za majumuisho kwenye shauri . Washtakiwa wote kwenye shauri hilo namba 112 la mwaka 2018 wanakabiliwa na mashtaka 13 yakiwemo kufanya kusanyiko na maandamano kinyume cha sheria na kutoa maneno ya uchochezi.