Iran yaathirika zaidi na Corona katika nchi za Mashariki ya kati

Iran leo imesema watu 54 zaidi walioambukizwa virusi vya Corona wamefariki na kuifanya idadi jumla ya waliofariki kutokana na ugonjwa huo nchini humo kufikia 291.

Kuna visa 8,042 vya maambukizi katika jamhuri hiyo ya kiislamu. Msemaji wa wizara ya afya Kianoush Jahanpour ametowa tangazo hilo kupitia mkutano na waandishi habari uliooneshwa kwenye televishhni.

Idadi ya waliokufa iliyotangazwa leo inaonesha ongezeko la asilimia 18 ya vifo ikilinganishwa na siku moja iliyopita.

Iran ndio nchi iliyoathirika kwa kiasi kikubwa na ugonjwa huo katika eneo la Mashariki ya kati.

Katika eneo hilo kuna zaidi ya visa 8,600 vilivyothibitishwa vya maambukizi ya virusi hivyo.

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu nchini Iran Javaid Rehman ameitaka nchi hiyo kuwaachia huru kwa muda wafungwa wote wa kisiasa, akisema inasikitisha kuwa na wafungwa wa kisiasa katika kipindi hiki cha mripuko wa virusi vya Corona.

Comments

Popular posts from this blog

Rais wa Marekani Donald Trump na Makamu Wake Huenda Wakapimwa Tena Corona Baada ya Mtumishi Mwingine Wa IKULU Kukutwa na Virusi Vya Corona

Mchezo wa Kwanza Wapigwa Marekani Bila Mashabiki

Mji mkuu wa Korea Kusini wafunga kumbi za starehe kwa hofu ya Corona