Hukumu ya Mbowe na viongozi wengine wa CHADEMA leo

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo March 10, 2020 inatarajia kutoa hukumu kwa Viongozi wa CHADEMA, wanaokabiliwa na kesi ya uchochezi Mahakamani hapo.

Viongozi wanaokabiliwa na shauri hilo ni pamoja na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, na Wabunge John Mnyika, Halima Mdee, Ester Bulaya, Ester Matiko, John Heche, Peter Msigwa na pia aliyekuwa Katibu Mkuu CHADEMA kabla ya kuhamia CCM, Vicent Mashinji.

Hukumu hiyo inakuja baada ya February 24, 2020 Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba kusikiliza ushahidi wa upande wa mashtaka na ule wa utetezi na kutoa siku tano za kazi kwa Mawakili wa pande zote mbili kuwasilisha hoja za majumuisho kwenye shauri .

Washtakiwa wote kwenye shauri hilo namba 112 la mwaka 2018 wanakabiliwa na mashtaka 13 yakiwemo kufanya kusanyiko na maandamano kinyume cha sheria na kutoa maneno ya uchochezi.

Comments

Popular posts from this blog

Rais wa Marekani Donald Trump na Makamu Wake Huenda Wakapimwa Tena Corona Baada ya Mtumishi Mwingine Wa IKULU Kukutwa na Virusi Vya Corona

Mchezo wa Kwanza Wapigwa Marekani Bila Mashabiki

Mji mkuu wa Korea Kusini wafunga kumbi za starehe kwa hofu ya Corona