Trump atarajiwa kutangaza mipango mipya ya kiuchumi

Rais wa Marekani Donald Trump anajiandaa kutangaza mipango ya kiuchumi itakayotowa mwelekeo utakaochukuliwa na taifa hilo kufuatia kuenea kwa virusi vya Corona.

Tangazo hilo linatolewa wakati masoko ya kiuchumi ya Marekani yakionesha kuporomoka kabla ya kufunguliwa kwa masoko.

Miongoni mwa hatua zinazofikiriwa ni kuundwa kwa sheria ya kuwalinda wafanyakazi wanaolipwa kwa masaa ambao wako katika hatari ya kukosa mshahara kutokana na kuyumba kwa shughuli za kiuchumi au hatua za kufungiwa kwenye Karantini.

Kadhalika rais Trump anafikiria hatua ya kuondowa kodi ya mshahara.

Ama kwa upande mwingine waziri wa ulinzi wa nchi hiyo Mark Esper ameakhirisha ziara yake ya kwenda India,Uzbekistan na Pakistan ili kusaidia katika usimamizi wa wizara hiyo katika kupambana na virusi vya Corona.

Comments

Popular posts from this blog

Rais wa Marekani Donald Trump na Makamu Wake Huenda Wakapimwa Tena Corona Baada ya Mtumishi Mwingine Wa IKULU Kukutwa na Virusi Vya Corona

Mchezo wa Kwanza Wapigwa Marekani Bila Mashabiki

Mji mkuu wa Korea Kusini wafunga kumbi za starehe kwa hofu ya Corona