Rais Putin aunga mkono marekebisho ya katiba ya Urusi
Rais Vladmir Putin wa Urusi amesema anaunga mkono pendekezo la marekebisho ya katiba ambayo yatamruhusu kugombea muhula mwingine wa kuendelea kukaa madarakani.
Putin ameunga mkono mapendekezo hayo yaliyowasilishwa na mbunge ambaye wakati wa utawala wa Soviet alikuwa mwanamke wa kwanza kusafiri anga za mbali.
Mbunge huyo amependekeza ama iondolewe kabisa sheria ya ukomo wa muhula wa rais madarakani au pafanyike marekebisho ya katiba yatakayomruhusu Putin agombee tena.
Msururu wa marekebisho ya katiba ya Urusi yatapigiwa kura nchi nzima mnamo tarehe 22 mwezi Ujao wa Aprili.
Rais Putin ameipinga hatua ya kuondolewa ukomo wa muhula wa rais lakini ameunga mkono fikra ya kufanyika marekebisho ya katiba.

Comments
Post a Comment