Mazishi ya Baba Kanumba Kufanyika Jumatano hii


Siku ya Machi 8, 2020 zilitoka taarifa za kifo cha Baba wa aliyekuwa staa wa filamu hapa nchini Steven Kanumba, aitwaye Charles Kanumba, aliyefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Mkoa wa Shinyanga.

 Happyness Charles ambaye ni mmoja wa watoto wa marehemu Baba Kanumba, akielezea kuhusu sababu ya kifo cha mzee huyo pamoja na ratiba kamili za mazishi ya msiba huo.

"Taratibu za mazishi yenyewe yataanza  kesho Jumanne, ambapo tutaaga mwili wa marehemu kuanzia saa 8 mchana kisha kuelekea nyumbani kwao Busega Mwanza, ambapo tutazikia siku ya Jumatano mida ya saa 7 mchana, halafu tutarudi kumalizia msiba nyumbani kwake Shinyanga"  ameeleza Happyness Charles.

"Baba ameanza kuumwa kichwa, tumbo na miguu kwa muda mrefu sana, alianza kuugua kabla ya Kanumba hajafariki kwa sababu alikuwa anaumwa polepole, kwahiyo kadri siku zinavyoenda hali inazidi kubadilika ghafla kisha akafariki" ameongeza

Comments

Popular posts from this blog

Rais wa Marekani Donald Trump na Makamu Wake Huenda Wakapimwa Tena Corona Baada ya Mtumishi Mwingine Wa IKULU Kukutwa na Virusi Vya Corona

Mchezo wa Kwanza Wapigwa Marekani Bila Mashabiki

Mji mkuu wa Korea Kusini wafunga kumbi za starehe kwa hofu ya Corona