RC Tabora aagiza kukamatwa kwa wanaotumia vyandarua kinyume cha utaratibu


MKUU wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amewaagiza viongozi wa vijiji na mitaa kuwamata watu wote watakutwa wakitumia vyandarua kwa matumizi mengine kando ya kujikinga na mbu.

Alisema matumizi ya vyandarua nje ya kujikinga na mbu yanapingana na juhudi za Serikali za kupambana malaria na kusababisha kupoteza nguvu kazi ya Taifa

Mwanri alitoa kauli hiyo  wilayani Kaliua wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Mkoa wa Tabora ziro malaria inaanza na mimi.

Alisema kuwa katika baadhi ya watu wanatumia vyandarua kuvulia samaki katika madimbwi na wengine wanatumia kuzungushia vifaranga vya kuku vishismbuliwe na mwewe.

Mwanri aliongeza kuwa kuna watu wengine wanatumia vyandarua hivyo kwa ajili ya kuzungushia bustani za matunda na mboga mboga ili kuzuia wadudu waharibifu.

Alisema matumizi hayo ambayo ni kinyume cha kujikinga na mbu ni marufuku mkoani na atakayekuwa atachukuliwa hatua.

Awali Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Honoratha Rutatatinisibwa alisema mwelekeo wa Serikali ni kuhakikisha kwamba ifikapo mwaka 2030 ugonjwa wa malaria uwe umetokomezwa.

Alisema takwimu zinaonyesha kiwango cha maambukizi ya ugonjwa wa malaria kwa Mkoa wa Tabora bado ni tatizo ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua ina asilimia 16.7 , kufuatia Uyui asilimia 16.1 na Sikonge ambayo ina asilimia 13.9.

Dkt. Rutatatinisibwa alisema Urambo ina asilimia 12.8, Manispaa ya Tabora asilimia 8.9, Halamashauri ya wilaya ya Nzega asimilia 8.7, Nzega Mji asilimia 6.8 na Igunga asilimia 5.6.

Alisema nguvu zaidi zinahitajika katika kupmbana na tatizo la malaria mkoani Tabora.

Comments

Popular posts from this blog

Mchezo wa Kwanza Wapigwa Marekani Bila Mashabiki

Mji mkuu wa Korea Kusini wafunga kumbi za starehe kwa hofu ya Corona

Rais wa Marekani Donald Trump na Makamu Wake Huenda Wakapimwa Tena Corona Baada ya Mtumishi Mwingine Wa IKULU Kukutwa na Virusi Vya Corona