Posts

Showing posts from May, 2020

Rais wa Marekani Donald Trump na Makamu Wake Huenda Wakapimwa Tena Corona Baada ya Mtumishi Mwingine Wa IKULU Kukutwa na Virusi Vya Corona

Image
Marekani imesema huenda Rais Trump na Makamu wake Mike Pence wakalazimika kupima tena corona kwa mara ya tatu mfululizo kufuatia Mfanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Katibu wa Habari) kuugua corona, juzi Viongozi hao walipimwa corona baada ya Mfanyakazi wa Ikulu kuugua corona. Trump mwenyewe ndiye  aliyetangaza siku ya Ijumaa wakati wa mkutano na wabunge na maseneta kutoka chama cha Republican kwamba Katie Miller, mke wa mshauri wake wa katika masuala ya uhamiaji, Stephen Miller, ambaye pia ni Msemaji wa Makamu wa rais wa Marekani Mike Pence ameathirika. Kutangazwa kwa kesi hii ya pili kwa siku mbili katika Ikulu ya White House kumezua hofu kwa afya ya rais na makamu wa rais, ambao wote wawili walianza tena shughuli zao na safari zao, wakati vifo vya watu waliofariki kwa Covid-19 vimezidi 80,000

Mji mkuu wa Korea Kusini wafunga kumbi za starehe kwa hofu ya Corona

Image
Mamlaka za mji mkuu wa Korea Kusini, Seoul zimeamuru kufungwa kwa maeneo yote ya kuuza vileo na kumbi za starehe baada ya kuzuka visa vipya vya virusi vya corona vinavyoibua wasiwasi wa kutokea wimbi la pili la kusambaa virusi hivyo hatari. A task force of economists and sociologists, as well as infectious-disease experts, drafted a 68-page “guidebook for distancing in daily life,” including installing partitions in dining-hall tables. Meya wa mji huo Park Won-soon amesema amri hiyo itakayoendelea bila kikomo imefuatia maambukizi mapya ya virusi vya corona yaligundulika kwenye wilaya ya Itaewon, yenye shughuli nyingi nyakati za usiku. Zaidi ya visa 24 vinahusishwa na mwanaume mmoja aliyegundulika kuwa maambukizi ya COVID-19 baada ya kutembelea kumbi tano za starehe kwenye wilaya ya Itaewon wiki iliyopita. Korea Kusini imekuwa mfano kwa jinsi ulimwengu unavyoweza kukabiliana na virusi vya corona, lakini meya wa mji wa Seoul ameonya uzembe unaweza kusababisha wimbi ji...

Vijana Nchini Kenya wavumbua mfumo wa CovIdent unaotarajiwa kutambua wenye virusi

Image
Tangu kuibuka kwa virusi vya corona, juhudi mbali mbali zimekua zikifanyika ili kuzuwia kusambaa kwa virusi ambavyo vinaambukizwa kwa kasi duniani na kusababisha vifo. Katika juhudi za Chuo kikuu cha Teknolojia cha Serikali cha Meru nchini Kenya kimevumbua mfumo wa kidigitali unaofahamika kama CovIdent utakaotoa alama za data binafsi kwa lengo la kurahisisha upimaji wa virusi vya corona kwa watu wengi. Uvumbuzi huu umefanywa na Wahandisi vijana Chuoni hapo wanaotambulika kama NaiTech chini ya usimamizi wa mhandisi Bundi Kotonya. Mfumo utasaidia kuwapa watu nafasi ya kupata, kunakili na kutumia matokea ya upimaji wao kwa njia rahisi. Mfumo huu utasaidia kuwatambua na kuwachuja wenye maambukizi ya virusi vya corona na hivyo kupunguza kuenea kwa Covid-19 ambapo baada ya mtu kufanyiwa vipimo vya corona mfumo utaweka alama maalumu ya siri (code) na kutuma maelezo yake katika kituo cha taifa cha udhibiti wa corona au ugonjwa mwingine ambapo maelezo hayo yatahifadhiwa. ''Alama...

Hapi Arejesha Gari la Mwalimu Aliyetapeliwa

Image
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Iringa katika kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Juni, 2020 imeweza kuokoa kiasi cha fedha zaidi ya shiliingi bilioni 1.2. Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Iringa, Mweli Kilimali amesema, katika kipindi hicho cha ufuatiliaji wa madeni ya wadaiwa sugu vyama vya akiba na mikopo (SACCOS) 67, vilifikiwa na zaidi ya bilioni 1.2 ziliokolewa. Mbali na fedha hizo pia amesema kuwa katika opresheni ya kuwatafuta wakopeshaji wa mikopo umiza, wamefanikiwa kukamata  gari lenye namba ya usajili T 311 DDF aina ya Nissan Serena iliyokuwa mali ya mwalimu mstaafu Hadija Nassor Mazola aliyekopa kiasi cha Mil 2 mwaka 2017 kutoka kwa mkopeshaji Micheal Wilson Sanga. Kwa upande, Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi ameipongeza TAKUKURU kwa kazi nzuri ya kuokoa fedha na mali za wananchi.

Mchezo wa Kwanza Wapigwa Marekani Bila Mashabiki

Image
Pambano la kwanza la ngumi tangu janga la Corona liingie nchini Marekani limepigwa usiku wa kuamkia leo Mei 10, 2020, ambapo Justin Gaethje amemchapa Tony Ferguson kwa TKO raundi ya 5 na kuibuka bingwa wa UFC interim lightweight. Pambano hilo limepigwa bila mshabiki kwenye uwanja wa VyStar Veterans Memorial huko Jacksonville, Florida. Awali pambano hilo lilitakiwa kupigwa 18 April huko Brooklyn lakini likaahirishwa kutokana na Janga la Corona na kupangiwa tarehe ambayo ni usiku wa Mei 10, 2020. Justin Gaethje mwenye miaka 31, amempiga Tony Ferguson mwenye miaka 36 na sasa ndio bingwa wa UFC Lightweight na atapigana na Khabib Nurmagomedov katika pambano ambalo litapangiwa tarehe baadaye mwaka huu.

Ndege Nyingine isiyo na Rubani ya Uturuki yatunguliwa Katika Anga ya Libya

Image
Wanamgambo wa jenerali muasi Khalifa Haftar wamesema kuwa wametungua ndege moja isiyo na rubani ya Uturuki kusini mwa mji mkuu wa Libya, Tripoli. Gazeti la al Rai al Yaum limeripoti habari hiyo na kusema kuwa, wanamgambo wanaojiita Jeshi la Taifa la Libya wanaoongozwa na jenerali muasi Khalifa Haftar, usiku wa kuamkia leo Jumapili wametangaza kuwa wametungua droni ya Uturuki aina ya "Bayraktar TB2" katika eneo la Ain Zara kwenye viunga vya kusini mwa Tripoli, mji mkuu wa Libya. Mara chungu nzima wanamgambo wa Jenerali Khalifa Haftar wamekuwa wakitangaza kutungua ndege zisizo na rubani za Uturuki katika anga ya Libya. Uturuki ambayo inaiunga mkono Serikali ya Mwafaka wa Kitaifa yenye makao yake mjini Tripli, Libya, imetuma wanajeshi wake nchini humo kwenda kuilinda serikali hiyo inayoongozwa na Waziri Mkuu Fayez al Sarraj kukabiliana na mashambulizi ya wanamgambo wa jenerali muasi, Khalifa Haftar. Khalifa Haftar anaongoza serikali ya mashariki mwa Libya na anaungwa mko...

Njia nyepesi na isiyo na gharama ya kuongea na mpenzi aliyekasirika

Image
Mara nyingi mitafaruko na kutokuelewana katika mahusiano huwa hakukwepeki hata iweje, hivyo endapo itatokea kutokuelewa katika mahusiano yenu, yaani mpenzi wako amekasirika  basi unatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo ili kuleta maelewanao; Mpunguze mhemko Hasira hujaza kifua, huathiri mzunguko wa damu na ufahamu. Mtu aliyekasirika huwa vigumu kwake kusikiliza au kutazama mambo kwa jicho la tatu. Mwenye hasira huwa hafikirii matokea yajayo badala yake hutazama zaidi tukio na jinsi ya kupata ushindi iwe kwa maneno au kwa mapambano. Katika hali ya namna hiyo, mtu mwingine akija na busara za kutaka kumgeuza haraka haraka hawezi kumuelewa. Muhimu hapo ni kuacha kumwadama, kujibizana naye, kumshawishi asikilize badala yake mpe nafasi ya kusema atakavyo, abwate ajuavyo huku wewe ukimuitikia na kumkubalia lawama zake. “Basi mpenzi mwenye makosa ni mimi.” Kauli za aina hii zitampunguza hasira kwani atajiona mshindi. Msome saikolojia yake Kwa kuwa unamfahamu mpenzi wako kwa kina itaku...

Kim Jong Un ajitokeza baada ya minong'ono kuhusu afya yake

Image
Kufuatia mbio ambazo ni za kiuchokozi katika majaribio ya makombora na silaha za nyuklia mwaka 2017,Kim alitumia michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi Korea kusini kuanzisha majadiliano na Marekani na Seoul mwaka 2018. Hatua  hiyo  ilisababisha  wimbi  la  mikutano, ikiwa  ni  pamoja  na mitatu  kati ya  Kim na  Trump. Lakini  majadiliano  hayo  yameshindwa  katika  miezi  iliyopita kutokana  na  kutokubaliana katika  kubadilishana  na  unafuu  wa vikwazo  pamoja  na  hatua za  kuachana  na  utengenezaji  wa silaha, ambao  ulizusha  shaka  juu  ya  iwapo  Kim kama ataondoa kabisa  hazina  yake  ya  silaha ambayo  anaiona  kuwa  ni nguzo yake  imara  ya  kuendelea  na  shughuli  zake. Kim aliingia  katika  mwaka  2020...

Klabu za ligi ya Uingereza kujadiliana kuhusu uwezekano wa kurejea viwanjani

Image
Klabu katika ligi kuu ya Uingereza zinatarajiwa kufanya mazungumzo leo kuhusu namna ya kumaliza msimu. Haya yanajiri huku mshambulizi wa Manchester City, Sergio Aguero, akikiri kuwa wachezaji wana wasiwasi kwamba wanaweza kuharakishwa kurudi viwanjani.  Ligi hiyo ya Uingereza inakabiliwa na kitisho cha kupata hasara ya euro bilioni moja ikiwa mechi hazitachezwa tena kwa sababu ya janga la corona. Suluhisho la hasara hiyo ni kuzicheza jumla ya mechi 92 ambazo zimesalia hata bila ya kuwepo mashabiki uwanjani.  Lakini ligi hiyo inakumbwa na changamoto nyingi za kimkakati katika majaribio yake kutaka kurejea viwanjani mnamo wakati Uingereza ikiwa kati ya mataifa yaliyoathiriwa mno na janga la COVID-19.

Rais wa Uturuki azungumza na wagonjwa wa virusi vya corona kwa njia ya video

Image
Rais Recep Tayyıp ErdoÄŸan azungumza kwa njia ya video na wagonjwa wa virusi vya corona wanaopatiwa  matibabu katika  hospitali  CerrahpaÅŸa. Taarifa iliztolewa katika ukurasa wake wa Twitter zimefahamisha kuwa rais ErdoÄŸan amezungumza na wagonjwa hao  baada ya kuongonishwa   kwa njia ya video na hospitali  hiyo . Waziri wa habari wa Uturuki Fahrettin Altun  na msemaji wa ikulu Ibrahim Kalın wameonekana katika picha iliorushwa ambapo rais ErdoÄŸan  alipokuwa akizungumza na wagonjwa hao.

Sumalee kuwakutanisha Alikiba na Diamond kwenye Qaswida

Image
Hitmaker wa Hakunaga, Sumalee,  aahidi kuwaleta wasanii Alikiba na DiamondPlatnumz kwenye Qaswida moja. Akizungumza leo Kupitia kipindi cha The Switch cha WasafiFm, Suma Lee amesema miongoni mwa mambo anayohitaji kuyatimiza ni kuwaimbisha Qaswida wakali wawili wa Bongo Fleva Alikiba na Diamond Platnumz "Nitaimba Qaswida na Diamond pamoja na AliKiba, iwe Qaswida moja ama kila mtu na ya kwake... wataimba iwe kilazima, kihiari, nitaimba nao. Wataimba Qaswida". Alisema Maalim Sumalee. Itakumbukwa, kabla ya kuachana na BongoFleva, SumaLee aliwahi kutamba na kibao chake cha Hakunaga lakini kwa sasa ana zawadi ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan aliyoiachiwa mapema wiki hii inaitwa YaRasulallah.

Diamond Platnumz Atangaza Habari NJEMA Kuhusu Wasafi FM

Image
Mkurugenzi Mkuu na CEO wa Wasafi Media Diamond Platnumz kupitia interview aliyoifanya kwenye Sports Arena amefunguka baada ya kuulizwa na Maulidi Kitenge kuhusu Wasafi Media kwenda mikoani. Amefunguka "Mwanzo tulikuwa hatujapa leseni ya Serikali kurushwa redio nchi nzima ila kwa mwaka huu tumeaminika na tumepewa leseni na Serikali kurushwa nchi nzima muda si mrefu tutaanza kurusha mikoani"

Mimi Mvrs Afunguka Kuhusu Dada Yake Vanessa MDEE Kuacha Kufanya Mziki na Kuendekeza Mapenzi

Image
Mimi Mvrs "Mimi Naona tu Mitandaoni wakisema kuwa dada yangu ameacha kufanya kazi yake ya muziki na yupo bize na Rotimi, Si kweli kazi anafanya na pia maisha mengine yanatakiwa yaendelee siyo kama muziki anaupa kisogo, hapana, wamuache afanye ambacho anajisikia kufanya" Tazama

Siri ya Utajiri wa Magari na Majumba wa Harmonize Yafichuka

Image
MARA baada ya msanii Rajabu Abdul, ‘Harmonize’ au Harmo kulamba dili la mamilioni kutoka Benki ya CRDB, baadhi ya watu ni kama walipigwa na shoti ya umeme na kubaki midomo wazi. Kwa mapana na marefu Risasi Mchanganyiko limepata siri kwa nini msanii huyo amepata dili hilo kubwa na siyo msanii mwingine yeyote Bongo. Akizungumza na mwandishi wetu mmoja wa mameneja wa Harmonize ajulikanaye kwa jina la Mchopa alisema: “Kilichombeba sana ni nidhamu, kujituma, kukubalika kwenye jamii, moyo wa uzalendo kwa taifa lake na ubora wa kazi zake.” Akizungumzia mpunga aliopiga msanii huyo, Mchopa alisema kuwa, ni fedha ndefu lakini akasita kuziweka kwenye ‘figa’ kwa sababu ya kuheshimu masharti yaliyopo kwenye mkataba wao na CRDB. Alisema, mpaka benki kubwa kama hiyo inampa mkataba Harmonize, ujue kuna utafiti wa kina umefanyika hadi kufika kwenye uamuzi huo. “CRDB siyo benki ndogo hapa nchini, ni benki kiongozi ya wazalendo na wajasiriamali wa nchi hii. “Ukiona wamemtambua msanii wetu, basi j...

Shehe Amuonya Sanchi Kubadili Dini "Kama Kweli Amebadili DINI Basi Afute Zile Picha za Kihasara"

Image
BAADA ya mwanamitindo mwenye umbo matata Bongo, Jane Rimoy ‘Sanchi’ kubadili dini na kuwa Muislam ambapo kwa sasa anajulikana kwa jina la Surraiya, Sheikh Ahmed Kandauma ameibuka na kumuonya, Risasi Mchanganyiko linakupa habari kamili. Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, shehe huyo alisema Sanchi kwa sasa anatakiwa kubadilika hasa kimuonekano, kwani awali kabla ya kubadili dini, alikuwa akivaa mavazi ya kubana na kumuonesha mwili wake ulivyo. Alisema dini ya Kiislam inataka heshima ya hali ya juu, kwani mambo ya kukaa nusu utupu na kujiachia kihasara ni kuidhalilisha dini, hivyo Sanchi anatakiwa kujilinda sana na mambo hayo kwa sasa kama kweli amekuwa Muislam afuate sheria na taratibu za dini. “Kwa sasa tunaendelea kumwangalia Sanchi kwa jicho lingine kama kweli amekuwa Muislam safi ambaye atafuata sheria za dini na kuachana na mambo yale ya zamani ya kukaa nusu utupu au kuvaa nguo zinazobana na kumwonyesha alivyozaliwa. “Kama kweli amebadili dini, basi anatakiwa kufuta hata ya...

Sababu ya Killy Kumsikiliza Mama yake Kutoka Kings

Image
Msanii Killy ambaye amejitoa katika lebo ya Kings Music Records, amesema ameamua kuchukua uamuzi huo kutoka kwa mama yake kwa sababu ndiyo mtu pekee aliyekuwa akimsapoti na anamfuatilia mienendo yake. Killy amesema hapendi  kuchanganya kazi zake na familia ila inapotokea suala kama hilo inabidi amsikilize mzazi, kwa sababu mama yake ndiyo mtu aliyekuwa anampa nauli tangu zamani na anataka aone faida anazozipata popote anapokuwepo. Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital  Killy amesema  "Suala la kutoka Kings Music lilianzia kwetu sisi kabla ya mtu yeyote kwa sababu tulikuwa na mambo yetu kichwani, japo mwanzo tulisema wazazi wetu ndiyo walichangia, Mama yangu ndiyo mtu ambaye alikuwa ananipa nauli tangu zamani, ananifuatilia mienendo yangu, popote nitakapokuwepo lazima ajue ninapata faida gani na kitu gani nafanya" "Ila nilimwambia mama yangu anipe sababu tatu za mimi kutoka Kings Music ila yeye akanipa tano, alivyoniambia nikainamisha kichwa chini mimi mwen...

Hamissa Mobetto Adai Kuwa Kwenye Mahusiano ya Pande Mbili

Image
Kwa wasanii wengi wa hapa nchini ukiwauliza kuhusu mahusiano yao watakujibu kwamba  yapo "private" yaani binafsi au mahusiano yao yapo "secrect" kwa maana yake ni ya siri. Sasa EATV & EA Radio Digital, imepiga stori na msanii Hamisa Mobetto ambaye amesema kwa sasa yupo kwenye mahusiano ya pande zote mbili kati ya hayo, pia ametueleza utofauti wa kuwa kwenye mahusiano binafsi na yale ya siri. "Sasa hivi nipo kwenye mahusiano na mtu fulani hivi wa kushangaza yaani amazing, na mahusiano yangu yapo katika pande zote mbili yaani binafsi na siri sidhani kama yatakuja kuwa mbele za watu, tofauti ya kuwa private ni mnaamua wenyewe kuwa hivyo ila watu wanajua kabisa kwamba mpo kwenye mahusiano" amesema Mobetto "Ila mahusiano ya siri ni yale ambayo mpo na mambo yenu binafsi na hakuna anayejua kama mpo kwenye mahusiano, ndiyo maana kwangu mimi nikasema mahusiano yangu yako katika pande zote mbili". ameongeza