Sababu ya Killy Kumsikiliza Mama yake Kutoka Kings


Msanii Killy ambaye amejitoa katika lebo ya Kings Music Records, amesema ameamua kuchukua uamuzi huo kutoka kwa mama yake kwa sababu ndiyo mtu pekee aliyekuwa akimsapoti na anamfuatilia mienendo yake.


Killy amesema hapendi  kuchanganya kazi zake na familia ila inapotokea suala kama hilo inabidi amsikilize mzazi, kwa sababu mama yake ndiyo mtu aliyekuwa anampa nauli tangu zamani na anataka aone faida anazozipata popote anapokuwepo.

Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital  Killy amesema  "Suala la kutoka Kings Music lilianzia kwetu sisi kabla ya mtu yeyote kwa sababu tulikuwa na mambo yetu kichwani, japo mwanzo tulisema wazazi wetu ndiyo walichangia, Mama yangu ndiyo mtu ambaye alikuwa ananipa nauli tangu zamani, ananifuatilia mienendo yangu, popote nitakapokuwepo lazima ajue ninapata faida gani na kitu gani nafanya"

"Ila nilimwambia mama yangu anipe sababu tatu za mimi kutoka Kings Music ila yeye akanipa tano, alivyoniambia nikainamisha kichwa chini mimi mwenyewe nikashindwa hata cha kuongea" ameongeza.

Comments

Popular posts from this blog

Rais wa Marekani Donald Trump na Makamu Wake Huenda Wakapimwa Tena Corona Baada ya Mtumishi Mwingine Wa IKULU Kukutwa na Virusi Vya Corona

Mchezo wa Kwanza Wapigwa Marekani Bila Mashabiki

Mji mkuu wa Korea Kusini wafunga kumbi za starehe kwa hofu ya Corona