Posts

Rais wa Marekani Donald Trump na Makamu Wake Huenda Wakapimwa Tena Corona Baada ya Mtumishi Mwingine Wa IKULU Kukutwa na Virusi Vya Corona

Image
Marekani imesema huenda Rais Trump na Makamu wake Mike Pence wakalazimika kupima tena corona kwa mara ya tatu mfululizo kufuatia Mfanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Katibu wa Habari) kuugua corona, juzi Viongozi hao walipimwa corona baada ya Mfanyakazi wa Ikulu kuugua corona. Trump mwenyewe ndiye  aliyetangaza siku ya Ijumaa wakati wa mkutano na wabunge na maseneta kutoka chama cha Republican kwamba Katie Miller, mke wa mshauri wake wa katika masuala ya uhamiaji, Stephen Miller, ambaye pia ni Msemaji wa Makamu wa rais wa Marekani Mike Pence ameathirika. Kutangazwa kwa kesi hii ya pili kwa siku mbili katika Ikulu ya White House kumezua hofu kwa afya ya rais na makamu wa rais, ambao wote wawili walianza tena shughuli zao na safari zao, wakati vifo vya watu waliofariki kwa Covid-19 vimezidi 80,000

Mji mkuu wa Korea Kusini wafunga kumbi za starehe kwa hofu ya Corona

Image
Mamlaka za mji mkuu wa Korea Kusini, Seoul zimeamuru kufungwa kwa maeneo yote ya kuuza vileo na kumbi za starehe baada ya kuzuka visa vipya vya virusi vya corona vinavyoibua wasiwasi wa kutokea wimbi la pili la kusambaa virusi hivyo hatari. A task force of economists and sociologists, as well as infectious-disease experts, drafted a 68-page “guidebook for distancing in daily life,” including installing partitions in dining-hall tables. Meya wa mji huo Park Won-soon amesema amri hiyo itakayoendelea bila kikomo imefuatia maambukizi mapya ya virusi vya corona yaligundulika kwenye wilaya ya Itaewon, yenye shughuli nyingi nyakati za usiku. Zaidi ya visa 24 vinahusishwa na mwanaume mmoja aliyegundulika kuwa maambukizi ya COVID-19 baada ya kutembelea kumbi tano za starehe kwenye wilaya ya Itaewon wiki iliyopita. Korea Kusini imekuwa mfano kwa jinsi ulimwengu unavyoweza kukabiliana na virusi vya corona, lakini meya wa mji wa Seoul ameonya uzembe unaweza kusababisha wimbi ji...

Vijana Nchini Kenya wavumbua mfumo wa CovIdent unaotarajiwa kutambua wenye virusi

Image
Tangu kuibuka kwa virusi vya corona, juhudi mbali mbali zimekua zikifanyika ili kuzuwia kusambaa kwa virusi ambavyo vinaambukizwa kwa kasi duniani na kusababisha vifo. Katika juhudi za Chuo kikuu cha Teknolojia cha Serikali cha Meru nchini Kenya kimevumbua mfumo wa kidigitali unaofahamika kama CovIdent utakaotoa alama za data binafsi kwa lengo la kurahisisha upimaji wa virusi vya corona kwa watu wengi. Uvumbuzi huu umefanywa na Wahandisi vijana Chuoni hapo wanaotambulika kama NaiTech chini ya usimamizi wa mhandisi Bundi Kotonya. Mfumo utasaidia kuwapa watu nafasi ya kupata, kunakili na kutumia matokea ya upimaji wao kwa njia rahisi. Mfumo huu utasaidia kuwatambua na kuwachuja wenye maambukizi ya virusi vya corona na hivyo kupunguza kuenea kwa Covid-19 ambapo baada ya mtu kufanyiwa vipimo vya corona mfumo utaweka alama maalumu ya siri (code) na kutuma maelezo yake katika kituo cha taifa cha udhibiti wa corona au ugonjwa mwingine ambapo maelezo hayo yatahifadhiwa. ''Alama...

Hapi Arejesha Gari la Mwalimu Aliyetapeliwa

Image
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Iringa katika kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Juni, 2020 imeweza kuokoa kiasi cha fedha zaidi ya shiliingi bilioni 1.2. Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Iringa, Mweli Kilimali amesema, katika kipindi hicho cha ufuatiliaji wa madeni ya wadaiwa sugu vyama vya akiba na mikopo (SACCOS) 67, vilifikiwa na zaidi ya bilioni 1.2 ziliokolewa. Mbali na fedha hizo pia amesema kuwa katika opresheni ya kuwatafuta wakopeshaji wa mikopo umiza, wamefanikiwa kukamata  gari lenye namba ya usajili T 311 DDF aina ya Nissan Serena iliyokuwa mali ya mwalimu mstaafu Hadija Nassor Mazola aliyekopa kiasi cha Mil 2 mwaka 2017 kutoka kwa mkopeshaji Micheal Wilson Sanga. Kwa upande, Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi ameipongeza TAKUKURU kwa kazi nzuri ya kuokoa fedha na mali za wananchi.

Mchezo wa Kwanza Wapigwa Marekani Bila Mashabiki

Image
Pambano la kwanza la ngumi tangu janga la Corona liingie nchini Marekani limepigwa usiku wa kuamkia leo Mei 10, 2020, ambapo Justin Gaethje amemchapa Tony Ferguson kwa TKO raundi ya 5 na kuibuka bingwa wa UFC interim lightweight. Pambano hilo limepigwa bila mshabiki kwenye uwanja wa VyStar Veterans Memorial huko Jacksonville, Florida. Awali pambano hilo lilitakiwa kupigwa 18 April huko Brooklyn lakini likaahirishwa kutokana na Janga la Corona na kupangiwa tarehe ambayo ni usiku wa Mei 10, 2020. Justin Gaethje mwenye miaka 31, amempiga Tony Ferguson mwenye miaka 36 na sasa ndio bingwa wa UFC Lightweight na atapigana na Khabib Nurmagomedov katika pambano ambalo litapangiwa tarehe baadaye mwaka huu.

Ndege Nyingine isiyo na Rubani ya Uturuki yatunguliwa Katika Anga ya Libya

Image
Wanamgambo wa jenerali muasi Khalifa Haftar wamesema kuwa wametungua ndege moja isiyo na rubani ya Uturuki kusini mwa mji mkuu wa Libya, Tripoli. Gazeti la al Rai al Yaum limeripoti habari hiyo na kusema kuwa, wanamgambo wanaojiita Jeshi la Taifa la Libya wanaoongozwa na jenerali muasi Khalifa Haftar, usiku wa kuamkia leo Jumapili wametangaza kuwa wametungua droni ya Uturuki aina ya "Bayraktar TB2" katika eneo la Ain Zara kwenye viunga vya kusini mwa Tripoli, mji mkuu wa Libya. Mara chungu nzima wanamgambo wa Jenerali Khalifa Haftar wamekuwa wakitangaza kutungua ndege zisizo na rubani za Uturuki katika anga ya Libya. Uturuki ambayo inaiunga mkono Serikali ya Mwafaka wa Kitaifa yenye makao yake mjini Tripli, Libya, imetuma wanajeshi wake nchini humo kwenda kuilinda serikali hiyo inayoongozwa na Waziri Mkuu Fayez al Sarraj kukabiliana na mashambulizi ya wanamgambo wa jenerali muasi, Khalifa Haftar. Khalifa Haftar anaongoza serikali ya mashariki mwa Libya na anaungwa mko...

Njia nyepesi na isiyo na gharama ya kuongea na mpenzi aliyekasirika

Image
Mara nyingi mitafaruko na kutokuelewana katika mahusiano huwa hakukwepeki hata iweje, hivyo endapo itatokea kutokuelewa katika mahusiano yenu, yaani mpenzi wako amekasirika  basi unatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo ili kuleta maelewanao; Mpunguze mhemko Hasira hujaza kifua, huathiri mzunguko wa damu na ufahamu. Mtu aliyekasirika huwa vigumu kwake kusikiliza au kutazama mambo kwa jicho la tatu. Mwenye hasira huwa hafikirii matokea yajayo badala yake hutazama zaidi tukio na jinsi ya kupata ushindi iwe kwa maneno au kwa mapambano. Katika hali ya namna hiyo, mtu mwingine akija na busara za kutaka kumgeuza haraka haraka hawezi kumuelewa. Muhimu hapo ni kuacha kumwadama, kujibizana naye, kumshawishi asikilize badala yake mpe nafasi ya kusema atakavyo, abwate ajuavyo huku wewe ukimuitikia na kumkubalia lawama zake. “Basi mpenzi mwenye makosa ni mimi.” Kauli za aina hii zitampunguza hasira kwani atajiona mshindi. Msome saikolojia yake Kwa kuwa unamfahamu mpenzi wako kwa kina itaku...